#HABARI: Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Elimu leo Januari 24, 2026, Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUCOHAS), Dkt. Bonny Betson, amesisitiza dhamira ya chuo hicho katika kuandaa wataalamu wa afya wenye weledi.
Amesema lengo ni kuhakikisha wahitimu wanakuwa na ujuzi wa hali ya juu utakaowawezesha kutatua changamoto za kiafya zinazowakabili wananchi katika mazingira yoyote nchini Tanzania.
Dkt. Betson ameeleza kuwa siri ya mafanikio ya MUCOHAS ni kuwashirikisha vijana kikamilifu katika mchakato mzima wa elimu, kuanzia uandaaji wa mitaala hadi utekelezaji wake.
Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa mafunzo wanayopata yanashabihiana na mahitaji halisi ya soko la ajira, pamoja na changamoto za kijamii, hivyo kuwajengea uwezo wa kutoa mchango chanya kwenye sekta ya afya.
Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo “Nguvu ya Vijana katika Kuunda Elimu ya Pamoja,” jambo ambalo Dkt. Betson anasema linatekelezwa kwa vitendo chuoni hapo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)