#HABARI: Mke wa kinara wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda Bobbi Wine, Barbie Kyagulanyi ameeleza mateso aliyoyapitia mikononi mwa watu anaodai ni maafisa wa usalama.

Bi Kyalunayi ambaye amelazwa katika hospitali moja mjini Kampala Uganda amesema kwamba, ‘ Ninajipa nguvu na kumuomba mume wangu asitoke mafichoni,’ alipohojiwa na wanahabari.

Wine amekuwa akiwaarifu wafuasi wake na dunia katika ukurasa wake wa mtandao wa X jinsi maafisa wa usalama waliovalia barakoa walivyoivamia nyumba yake na kuharibu vitu kabla ya kuwachapa waliokuwa ndani akiwemo mke na watoto wake.

Awali Wine alihisi kuhofia usalama wa mke wake ambaye alisema alikuwa amefungiwa katika chumba kimoja na wala hakujua madhumuni ya maafisa hao yalikuwa yapi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *