Rais wa Shirikisho la soka la Ujerumani (DFB), amesema ni wakati wakati wa kujiondoa kwenye Kombe la Dunia la 2026 kutokana na hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump.

Marekani itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia msimu wa joto mwaka huu, ikishirikiana na Canada na Mexico.

Mapema mwezi huu, Rais Trump aliwakasirisha viongozi wa Ulaya kuhusu azma yake ya kutwaa kisiwa cha Greenland, ambacho sasa kinasimamiwa na Denmark.

Marekani ni mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia ikishirikiana na nchi za Canada na Mexico. Marekani itakuwa mwenyeji wa mechi 78 kati ya 104 za mashindano hayo.

Itakumbukwa kuwa Marekani iliwahi kuzihimiza nchi nyingine kususia michezo ya Olimpiki ya 1980 kwa sababu ya Muungano wa Kisovieti kuivamia Afghanistan.

Wakati huo huo, kura ya maoni ya hivi karibuni iliyofanywa na Taasisi ya INSA imefichua matokeo ya kushangaza; 47% ya Wajerumani wameunga mkono wazo la kususia Kombe la Dunia FIFA 2026 iwapo Washington intanyakua eneo la Greenland, ikilinganishwa na 35% waliopinga wazo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *