Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amepuuza madai ya hivi karibuni kwamba takriban watu 30,000 waliuawa wakati wa ghasia zilizoungwa mkono na wageni za hivi karibuni nchini Iran.

Baqaei alisema jana Jumapili kwamba takwimu hiyo, ambayo ilionekana katika chapisho la hivi karibuni kwenye mtandao wa X na Open Source Intel, inakumbusha mbinu zilizotumika katika Ujerumani ya Nazi chini ya utawala wa Adolf Hitler, ambaye alitegemea kukaririwa pasina kukoma kwa “Uongo Mkubwa.”

“UONGO MKUBWA wa mtindo wa Hitler: je, hii si idadi waliyopanga kuua katika mitaa ya Iran?!” amesema Baqaei katika chapisho kwenye akaunti yake ya X.

Alikuwa akiashiria ripoti zinazosema waandamanaji wanaoungwa mkono na nchi za kigeni walitaka kuua idadi kubwa ya raia na kuitupia serikali lawama ya mauaji hayo.

Ameongeza kuandika: “Hata hivyo, walishindwa, na sasa wanajaribu Kusambaza habari feki kwenye vyombo vya habari. Ni uovu halisi!” 

Takwimu rasmi za serikali ya Iran zinaripoti kwamba zaidi ya watu 3,000 waliuawa katika ghasia na hujuma za kigaidi zilizofadhiliwa na kusaidiwa na mashirika ya ujasusi ya Marekani na Israel katika miji na vijiji vya Iran mapema mwezu huu wa Januari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *