#HABARI: Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) imeendelea kuwa chachu ya maendeleo nchini, ikirahisisha usafiri wa abiria na mizigo, sambamba na kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii.
Hali hiyo imejitokeza baada ya mashabiki wa Klabu ya Esperance De Tunis kutoka Tunisia kuonekana katika Stesheni ya SGR Magufuli, Dar es Salaam, wakisafiri kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro kwa shughuli za utalii.
Tukio hilo limeonesha namna SGR inavyochangia kukuza utalii wa ndani na wa Kimataifa, huku wageni wakitumia fursa ya uwepo wao nchini kutembelea vivutio mbalimbali kabla ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Esperance De Tunis na Simba SC, unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
SGR, ambayo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na kuendelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuthibitisha mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa kupitia usafiri wa kisasa, salama na wa uhakika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.