#HAARI: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Bi Mwajuma Nasombe, amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Kimataifa cha Ngangamfumuni kuongeza kasi ya ujenzi kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kabla ya Aprili 20 mwaka huu.
Agizo hilo amelitoa baada ya kubaini kasi ya utekelezaji wa mradi huo imekuwa ya kusuasua na kutoa malekezo hayo wakati wa ziara ya ukaguzi aliyofanya katika eneo la mradi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Manispaa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wao, Wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wamesema wataongeza nguvu kazi, vifaa pamoja na muda wa kazi kwa kufanya zamu ili kukamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.