Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchi nzima, imepelekea mchezo kati ya Simba na TRA United kuahirishwa kutokana na Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji.
Mchezo huo ulipangwa kuchezwa saa 10:jioni ukiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Bara
Kwa mujibu wa Kamishina wa mchezo huo, Mussa Nyamandege ameahirisha mchezo huo akitumia sheria namba moja ya Uwanja.
”Kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha Uwanja umejaa maji mpira hauwezi kudunda mimi kama kamishina wa huu wa mchezo nausitisha mchezo mpaka hapo utakapopangiwa siku nyingine, kabla ya kufanya maamuzi nimewaita viongozi wa pande zote mbili TRA United na Simba pamoja na waamuzi tukakubaliana kupitia sheria namba moja ya Uwanja.” Amesema.
Ikumbukwe inakuwa mara ya tatu sasa mchezo kati ya timu hizo mbili kuahirishwa awali huko nyuma ilikuwa upigwe Oktoba 30, 2025 ikaahirishwa mpaka Desemba 3, ilipofika hiyo tarehe ikaahirishwa tena kutokana na sababu tofauti tofauti.

(Feed generated with FetchRSS)