Zaidi ya Watanzania milioni nane, hususan vijana, wanatarajiwa kunufaika na ajira za moja kwa moja ifikapo mwaka 2030 kupitia mradi wa kituo cha pamoja cha kuwezesha manunuzi na kusaidia mauzo ya bidhaa nje ya nchi, pamoja na programu ya mafunzo kwa wawekezaji vijana iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema mpango huo umeanzishwa kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kuwa wawekezaji na wazalishaji wenye ushindani katika soko la kimataifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi nchini (TISEZA), Gilead Teri amesema maeneo ya kiuchumi yanatarajiwa kuwa nyezo ya ukuaji wa viwanda na teknolojia.

#AzamTvUpdates
✍️ Upendo Michael
Mhariri | @rajjmsangi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *