Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 12 ambacho kilikuwa katika hatari ya kufanyiwa ubadhilifu, wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Kwedihwahwala, iliyopo Kata ya Mgambo, Wilaya ya Handeni. Fedha hizo zilitolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa chumba kimoja cha darasa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Mariam Mayaya amesema kuwa taasisi hiyo ilibaini kuwepo kwa mapungufu ya viwango vya ujenzi katika hatua za umaliziaji wa jengo hilo.

Kutokana na hali hiyo, TAKUKURU iliwasiliana na mamlaka husika na kusababisha kazi hiyo kurudiwa upya ili kuhakikisha inakidhi viwango stahiki na kuendana na thamani halisi ya fedha iliyotumika.
#startvupdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *