Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wamekumbushwa kuzingatia misingi na kanuni za maadili ya utumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao.

Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Hamad Bakari amesisitiza viongozi hao pia kuzingatia matumizi sahihi ya taarifa; kuepuka vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka au wadhifa; kuepuka kutumia mali ya umma kwa maslahi binafsi na kulinda haiba wakati wa kazi na baada ya kustaafu.

Mnapaswa kujali wateja wa nje na ndani, kuheshimiana na kuheshimu haki za faragha, lakini pia mnapaswa kutoa huduma kwa wakati.”

Bakari pia amewasisitiza watumishi hao kujali muda wa kazi, kutoa huduma pasipo upenedeleo, kufanya kazi kwa ufanisi na kutokutoa taarifa kwa watu wasiohusika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Ziwa, CPA Janet Nyoni akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Baraza walioshiriki katika semina hiyo ameahidi kuzingatia yote waliyokumbushwa katika kutimiza majukumu yao ya kuhudumia umma.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *