Rais wa Marekani Donald Trump amesema nchi “kama Uingereza’ ambazo haziwezi kupata mafuta ya ndege kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa kuhusiana na Mlango Bahari wa Hormuz zinapaswa “kuwa na ujasiri ambao umeshachelewa, kwenda kwenye Mlango Bahari, na KUCHUKUA tu’.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Truth Social, aliandika kwamba nchi “zitalazimika kuanza kujifunza jinsi ya kujipigania, Marekani haitakuwapo kuwasaidia tena, kama vile ambavyo hamkuwepo tulipowahitaji.” akizungumzia nchi “‘ambazo zilikataa kushiriki katika vita vya lIran”.

“Kimsingi, Iran imeangamizwa kabisa. Sehemu ngumu imekamilika, ujumbe huo uliongeza, ukiishia na: “Nendeni mukachukue mafuta yanu mwenyewe!” Ufaransa ‘haisaidii sana, Trump asema katika ujumbe uliofuata

Katika ujumbe uliofuata alioutuma kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema Ufaransa “haikuruhusu ndege zinazoelekea Israel, zenye vifaa vya kijeshi, kupaa juu ya eneo la Ufaransa”. Aliendelea kusema Ufaransa “imekuwa haina msaada wowote kwa ‘Iran anayechinja watu, ambayo imesambaratishwa!”

Ujumbe huo unahitimishwa na rais wa Marekani akisema: “Marekani ITAKUMBUKA!!!”

#Chanzobbcswahili
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *