Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imetumia Sh25 bilioni kujenga Kituo cha Kupoza Umeme 1x20MVA, 220/33kv pamoja na njia za kusambaza Umeme katika Wilaya ya Kilombero.

kukamilika kwa ujenzi huo kumeboresha upatikanaji wa umeme na kuondoa changamoto ya kukatika kwa nishati hiyo katika wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi na kuchochea ukuaji wa uchumi hususani shughuli za kijamii, viwanda, kilimo na madini.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Machi 31, 2026 wakati wa ziara ya wahariri waliotembelea mradi huo kujionea utekelezaji na tija yake kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika ukanda wa Morogoro Kusini.

“Fursa za uwekezaji wilayani hapa zimeongezeka baada ya kukamilika kwa kituo hiki, ninatoa wito kwa wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwani tunao umeme wa uhakika na toshelevu,” amebainisha Wakili Kyoba.

Kwa upande wake, Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya Kusambaza Umeme kutoka REA, Mhandisi Deogratius Nagu, amesema gharama za mradi huo zinahusisha pia usimikaji wa mashine umba (transfoma) pamoja na mifumo yake ya uendeshaji, udhibiti na ulinzi, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme za msongo wa kilovolti 33 zenye urefu wa kilometa 70 pamoja na gharama za mshauri elekezi.

“Kituo hiki kimeondoa changamoto ya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Kilombero na Ulanga na kuwezesha wananchi kuendeleza shughuli za uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao,” alisema Nagu.

Naye Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amesema uwekezaji huo unaonesha matumizi sahihi ya rasilimali za umma na mchango wa REA katika kusambaza huduma ya umeme vijijini.

Balile amesema REA imeonyesha mfano wa kipekee kwenye utekelezaji wa majukumu yake na kwamba kazi iliyokwishakamilika ni kubwa na manufaa yake yanaonekana na ametoa wito kwa Taasisi zingine za Serikali kuiga mfano huo.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *