#HABARI: Kufuatia sintofahamu inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini juu ya baadhi ya wanaume kudai kushikwa bega na kuchukuliwa nyeti zao kwa mazingira tatanishi, matukio ambayo yanahusishwa na imani za kishirikina, Afisa Polisi Jamii Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Mrakibu wa Polisi Anyelwisye Mwakasungula, ameonya jamii kuacha kuzusha taharuki na kueneza taarifa zisizo na ukweli zinazohusiana na imani potofu.
Mwakasungula amesema kuwa vitendo vya kusambaza taarifa za uongo vinasababisha hofu kwa wananchi na kuvuruga amani ya jamii bila sababu za msingi.
Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuepuka vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, huku akiwataka kuripoti matukio yoyote ya uhalifu kupitia njia rasmi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.
“Yeyote atakaye sababisha taharuki ya namna hiyo tutamkamata, wale wameshakamatwa watafikishwa mahakamani, ili sheria ichukue mkondo wake, hatuwezi kuacha watu wakafanya mambo ya kihuni kama yale, shughuli zilisimama hapa mandela kwa sababu ya taharuki kwamba mtu kachukuliwa nyeti zake”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)