
Wanasiasa 42 kutoka vyama mbalimbali wapo kizuizini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanasiasa hao wamekamatwa na kuzuiwa na maafisa wa Inteljensia nchini humo na hali zao za kibinadamu zinaendelea kuwa mbaya.
Idadi kubwa ya wanasiasa waliokamatwa ni kutoka upinzani, wakiwemo wanasiasa 20 kutoka chama cha Ensemble pour la République kinachoongozwa na Moïse Katumbi, wanne kutoka chama cha PPRD chake rais wa zamani Joseph Kabila, akiwemo Emmanuel Shadary na Aubin Minaku, wameendelea kuzuia jela tangu mwezi Januari kwa kuikosoa serikali ya rais Felix Tshisekedi.
Aidha, ripoti hii inayotolewa kila mwezi inaeleza kuwa, mbai na wanasiasa waliokamatwa, visa 439 vya haki za binadamu, vimekiukwa nchini DRC tangu mwezi Januari mwaka huu.
Aidha, ripoti hiyo imebaini kuwa makundi yenye silaha, yamehusika pakubwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu yakiwemo mauaji ya raia wa kawaida.