Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji Tanzania (TASEZA), Gilead Teri, amesema serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kusaidia wawekezaji wazawa kukuza mitaji yao na kuwekeza kwa urahisi zaidi nchini.
Ameeleza kuwa miongoni mwa hatua hizo ni kutoa nafuu ya kodi na kupunguza baadhi ya makato kwenye malighafi zinazotumika katika uzalishaji, hatua inayolenga kupunguza gharama za uendeshaji kwa wawekezaji wa ndani.
Aidha, serikali imechukua jukumu la kugharamia baadhi ya tozo ambazo zingemlazimu mwekezaji kutumia fedha nyingi, ili kulinda mitaji yao na kuwapa nafasi ya kuwekeza zaidi. Hatua hiyo inatarajiwa kuchochea ukuaji wa sekta binafsi na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini.
#AzamTVUpdates
✍Ibrahim Kulumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
@balqis_njuki
@goodluckpaul_mc
(Feed generated with FetchRSS)