#HABARI: Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kuwaokoa watu nane waliokuwa wamezingirwa na maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko.
Tukio hilo limetokea leo Aprili 11, 2026 majira ya saa 07:45 asubuhi katika kijiji cha Koboko Kusini Kata ya Nasai wilayani Siha, baada ya maji kuingia kwenye makazi ya wananchi na kuwazuia kutoka nje.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kituo cha Siha, Askari walifika eneo la tukio kwa wakati na kuanza operesheni ya uokoaji, ambapo walifanikiwa kuwaokoa watu wote waliokuwa wamekwama ndani ya nyumba zilizozingirwa na maji.
Waliookolewa ni watu wazima wawili pamoja na watoto sita, wote wakiwa wa jinsia ya kike, huku kaya nne zikiathirika na tukio hilo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)