Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Njelu, amesema wingi wa mamlaka za udhibiti na kodi mbalimbali nchini unachangia kudhoofisha uwekezaji na ukuaji wa biashara.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni Dodoma, Njelu amesema wawekezaji na wafanyabiashara wanakabiliwa na mzigo mkubwa wa tozo na taratibu nyingi kutoka taasisi tofauti za serikali.
Amesema hali hiyo inapunguza motisha ya uwekezaji na kuathiri mazingira ya biashara nchini.
Njelu ameishauri serikali kupitia upya mifumo ya udhibiti na uratibu wa kodi ili kurahisisha mazingira ya uwekezaji na kukuza uchumi.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)