Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu Fred Vunjabei, ameongoza kura za maoni katika uchaguzi wa ndani wa Jimbo la Isimani.
Fred amewashinda makada wenzake 17 ambako jumla ya wanachama 18 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge jimbo hilo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Utaratibu na Wenye Ulemavu), William Vangimembe Lukuvi aliyefariki dunia.
Vunjabei ameongoza uchaguzi huo kwa kupata kura 2,703 na kuwabwaga wagombea 17.
Nafasi ya pili imechukuliwa na Festo Kiswaga aliyepata kura 873 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mkuu wa Wilaya (DC), Emmanuela Mtatifikolo, aliyepata kura 621.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)