Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi kwa kufikisha nishati ya umeme vijijini kupitia Usambazaji wa Nishati ya Umeme pamoja na Nishati Safi ya kupikia.
Akitembelea banda la REA katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma Waziri Ndejembi amesema wataalam wa REA wanatekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya kuwafikishia wananchi kote nchini nishati.
Ndejembi amewaalika wabunge kutembelea Banda la Maonesho la Nishati ili kushuhudia kazi kubwa inayotekelezwa na Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake.
Amesema taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinashiriki na kwamba wataalam wapo tayari na ni fursa kwa Wabunge kukutana na wataalam hao ili kujadili changamoto zilizopo na kutazama namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa REA, mhandisi Hassan Saidy amemhakikishia Waziri Ndejembi kuwa, miradi yote inayotekelezwa kwa sasa itakamilika kwa wakati na REA imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi hiyo.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki katika Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Aprili, 2026.

(Feed generated with FetchRSS)