Rais Samia Suluhu Hassan, ameagiza kutengwa na kuendelezwa maeneo rasmi kwa shughuli za mama na baba lishe ili kuboresha mazingira yao ya kazi.
Ametoa agizo hilo Aprili 21, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la kitaifa la kundi hilo, akimtaka Waziri wa TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, kushirikiana na wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha maeneo hayo yanapatikana nchi nzima.
Rais Samia pia amesisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu ya kufanyia biashara, ikiwemo matumizi ya nishati safi na mazingira rafiki kwa wafanyabiashara hao.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)