
Maafisa wa juu wa serikali ya Iran, wanaishtumu Marekani kwa kukwamisha mchakato wa mazungumzo ya amani, kufuatia hatua yake ya kuzuia meli za Iran kwenye mlango wa Bahari wa Hormuz na shughuli katika bandari zake.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema, nchi yake inahitaji mazungumzo na maelewano ya kweli lakini jitihada zake zinazuiwa na hatua ya Marekani kuendelea kuzuia meli zake.
Wakati viongozi wa Iran wakisema hayo, jeshi lake la wanamaji, limesema limekamata na kuzuia meli mbili katika mlango huo wa Bahari na kushambulia meli ya tatu, kwa kukiuka utaratibu katika mlango huo wa Bahari.
Nao wanajeshi wa majini wa Marekani, wameingia kwenye meli ya Iran iliyokuwa inasafirisha mafuta kwenye Bahari Hindi, huku Iran ikisema imepokea malipo ya Kwanza kutoka kwenye ada inayotoza kwenye mlango wa Bahari ya Hormuz.
Katika hatua nyingine, rais Donald Trump amewaagiza wanajeshi wa nchi yake kuwapiga risasi na kuwauwa watu watakaojaribu kutega mabomu kwenye mlango wa Bahari ya Hormuz, akisisitiza kuwa wanajeshi wake wanadhibiti kikamilifu ĂȘneo hilo la Bahari.