Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu Amani Oktoba 29, imesema ushahidi iliyokusanywa ulibaini vijana wasiopungua 500 walihifadhiwa msituni, makambi na maeneo mbalimbali nchini kwa siku 28 ili kufanya ghasia Oktoba 29.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othman Chande wakati akiwasilisha ripoti ya tume hiyo kwa Dkt Rais Samia Suluhu Hassan leo Ikulu Dar es Salaam.
“Tume kupitia uchunguzi wake ilibaini mojawapo ya nyumba hizo iliyopo Dar es Salaam ambayo ina umbali wa takribani mita 10 kutoka kituo cha polisi,” amesema Jaji Chande

Jaji Chande amesema pamoja na Tume kupokea ushahidi unaonyesha viasharia vya uwepo wa mpango wa kuvurugu siku ya uchaguzi mkuu, lakini hakuna ushahidi wa hatua stahiki kuchukuliwa kikamilifu kabla ya matukio ya uvunjifu wa amani.

“Kama nilivyoeleza awali wafanya ghasia walitumia mbinu mbalimbali ambazo hazikutarajiwa na mbinu hizo ni pamoja na kufanya uvunjifu wa amani kwa wakati mmoja katika sehemu mbalimbali kwa kutumia mbinu mtawanyiko,” amesema Jaji Chande.

#RipotiYaTume #UkweliOkt29

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *