Watu 518 walipoteza maisha wakati wa vurugu za uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Tanzania tarehe 29 mwezi Oktoba mwaka uliopita, kwa mujibu wa ripoti ya tume ya uchunguzi ambayo imewasilisha ripoti yake hivi leo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman, amesema kati ya watu hao 518 waliouawa, 490 walikuwa ni wanaume.

Aidha, ameeleza kuwa, uchunguzi wao umebaini kuwa vurugu hizo zilipangwa.

Hii ndio mara ya kwanza takwimu za mauaji ya vurugu hizo zinawekwa wazi, licha ya upinzani kudai kuwa watu kati ya 1,000 hadi 2,000, waliuawa.

Ripoti ya Tume hiyo, pia imebaini kuwa, haikupata ushahidi iwapo kulikuwa na kaburi la pamoja ambalo watu waliouwa walizikwa, huku ikieleza kuwa baadhi ya picha za vurugu hizi hazikuwa halisi na zilitengezwa na akili unde AI.

Rais Samia Suluhu Hassan, akipokea ripoti hiyo, amevilaumu vyombo vya Habari vya Kimataifa na vya nje, kupotosha kilichotokea wakati wa vurugu hizo.

Wakati tume hiyo ikipendekeza maridhiano ya kitaifa baada ya vurugu hizo, chama kikuu cha upizani CHADEMA ambacho kiongozi wake Tundu Lissu ameendelea kuzuiwa jela kwa tuhuma za uhaini, kilisema hakina imani na Tume hiyo na matokeo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *