Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Ushetu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Emmaneul Cherehani ameiomba serikali kupitia Wizara ya Nishati kuwekeza miundombinu na umeme wa uhakika katika vijiji, Kata na maeneo mengine yenye makusanyo makubwa ili Watanzania waweze kufanya uwekezaji wenye tija, kuongeza mapato na kunufaika na kazi zinazofanywa na Serikali.

Cherehani ameeleza hayo bungeni Dodoma Aprili 22, 2026 wakati Wizara ya Nishati iliposoma bajeti ya mwaka 2026/2027 ndani ya bunge hilo.

Awali ameshukuru serikali kuputia wizara hiyo kwa kutekeleza mradi wa kufua umeme wa jua uliogharimu kiasi cha Sh bilioni 11 uliopo katiak Kijiji cha Kayenze Kata ya Ukune katika Halamashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Amesema pamoja na utekelezaji huo bado anaiomba wizara hiyo kutimiza ahadi ya kituo cha kupoozea umeme liyompatia  miaka mitatu iliyopita akifafanua kuwa amepokea vijiji 112 vina umeme tayari na katika vitongoji 554 vya kwenye Jimbo lake tayari vitongoji 285 vina umeme na wamempa vitongoji 136 ameomba vitongoji 145 vibaki wamalizie ili wananchi waweze kunufaika na kazi za Rais Samia.

Pia amesema ameomba wizara hiyo ifanikishe upatikanji wa nishati kubwa na za uhakika katika kata zenye makusanyo na mapato makubwa katika jimbo lake kwani kutokuwa na umeme wa uhakika kumekuwa kukikwamisha shughuli zao za uwekezaji na uzalishaji hususani katika eneo la Mwabomba ambalo wananchi wengi hujenga viwanda.

“Naomba mtuletee transfoma zenye uweze mkubwa mimi hapa niliomba Mkoa wa Kitanesco Kahama, alisema Kahama inahitaji mkoa wa Tanesco makusanyo ya Kahama tunakusanya zaidi ya Sh7.370 bilioni na kwa mwaka wanakusanya zaidi ya bilioni 90 na kwa miaka mitatu ni zaidi ya milioni 290 lakini kuna miundombinu mibovu, umeme unakatika kila mara na biashara za watanzania katika halmashauri zetu tatu imekuwa na biashara kubwa sana ya jenereta kuliko kulipia umeme,” ameeleza Cherehani.

Ameongeza kuna eneo linaitwa Dodoma kuna vijana zaidi ya 3000 wametengewa eneo lao wamewekeza lakini changamoto na kilio chao ni kukatika katika kwa umeme hali ambayo imekuwa ikiwasababishia hasara na mashine zao kuungua.

“Embu njoo fanya ziara Kahama mheshimiwa Waziri njoo uione kwa macho unapoiona wafanyabiashara, benki kubwa 13 ziko pale ni lango la biashara kwa nchi za Afrika Mashariki kwani kwa siku inapitisha magari zaidi ya 300 makubwa na yanayo lala pale ni ya kutosha kwahiyo, kwahiyo ukituwekea mkoa wa Kitenesco kwa eneo unalo kusanya Sh90 bilioni kwa mwaka na Sh280 bilioni kwa miaka mitatu ukiweka umeme usio katika utakusanya fedha kiasi gani,” ameeleza Cherehani.

Ameshauri serikali kuwekeza umeme wa kutosha na kukarabati miundombinu kwa imara katika maeneo yenye makusanyo makubwa ili kuongeza mapato zaidi yenye tija.

Pia ameshauri watoe nafasi kwa wabunge wenye dhamana na majimbo husika kuwasha umeme wenyewe iki waweze kuoata nafasi ya kumsemea Rais na kuisema siasa kwnai ndiyo waliokuja kuomba umeme kwa ajili ya wananchi wao na kushuhudia utekelezaji wa bajeti waliyoimba ndani ya bunge hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *