Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amefungua mafunzo ya siku tatu yenye lengo la kuwajengea uelewa wataalamu wa TARURA kutoka TAMISEMI, ofisi ya Makao Makuu, Mikoa, Wilaya, Mhandisi Mshauri pamoja na Mkandarasi katika kutekeleza mradi wa Sanifu na Jenga wa barabara zinazoingia uwanja wa AFCON jijini Arusha.

‎Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhandisi Seff amesema lengo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa miradi ya sanifu na jenga ili kuimarisha uzingatiaji wa taratibu, kushughulikia changamoto kwa wakati na kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa mafanikio.


‎Mhandisi Seff amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa TARURA, Wakala huo haujawahi kupata mradi mkubwa kama huo, hivyo mafunzo hayo ni fursa muhimu ya kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani ili wawe tayari kushughulikia miradi mikubwa zaidi ijayo.

‎Amewakumbusha wasimamizi wa mradi kuzingatia muda akieleza kuwa barabara hizo zinatakiwa kukamilika ifikapo Mei 2027 bila nyongeza ya muda.

‎“Serikali imeiamini TARURA kwa kuipatia jukumu hilo kwa manufaa ya Taifa hivyo hamna budi kufanya kazi usiku na mchana.”

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *