SINGIDA Black Stars imekuwa timu ya kwanza kutoka LIgi Kuu Bara kutolewa kwenye mashindano ya Muungano ikiishia hatua ya robo fainali baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mlandegelakini wakaziacha lawama kwa mwamuzi wa mchezo huo Mfaume Nassoro.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Singida Black Stars, Muhibu Kanu, amesema hawakutarajia kupata matokeo ya kutolewa mapema lakini ni kama wamesababishiwa hilo na mwamuzi wa mchezo huo Mfaume.

Kanu amesematimu yake ilikuwa inaumizwa kwenye matukio mengi ikiondolewa utulivu na mwamuzi huyo akionyesha wazi kwamba alitamani kuwaona Mlandege ikipata ushindi huo.

MLA 01

Kocha huyo amesemakuwa Singida ni kama imeondolewa kwa nguvu kwenye mashindano hayo ambapo matukio mawili ya penalti za wazi Mfaume alishindwa kufanya maamuzi na kuwacha Mlandege wakinufaika.

“Kuna wakati unakubaliana na matokeo ambayo unakutana nayo hasa pale ambapo timu yako haijacheza vizuri lakini hiki kilichotokea jana ni wazi mwamuzi alikuwa na ajenda yake binafsi na sio kufuata sheria 17 za soka,” amesemaKanu.

“Timu inatengeneza nafasi Mlandege wanacheza vibaya lakini mpia bado upo kwetu tunakwenda kushambulia unamuona mwamuzi anasema turudishe nyuma tucheze faulo, hiyo ni sheria gani?

MLA 02

“Wachezaji wangu wanachezewa vibaya mara mbili kwenye eneo la hatari tena akiwa anaona akiwa karibu kabisa anaacha, kwahiyo ni kama alikuwa anataka kuwabeba Mlandege waingie nusu fainali na sisi Singida hatutakiwi.”

Kanu amesema wanarudi nyumbani kujiandaa na muendelezo wa ligi ambapo watapata muda wa kujipanga na mechi zinazofuata baada ya kuondolewa kwenye ligi ya Muungano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *