Serikali imewaagiza wawekezaji nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa, hususan vijana na wanawake, ili kuongeza ujuzi wa vitendo na kukuza uchumi wa viwanda.
Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Waziri Salum, akiwa mkoani Tanga katika ziara ya kikazi.
Amesema uwekezaji wenye tija ni ule unaozalisha ajira kwa Watanzania na kuwezesha uhamishaji wa teknolojia.
Katika ziara hiyo, ametembelea viwanda vya Neelkanth na Tanga Cement, ambako alijionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto za wawekezaji.
Kiwanda cha Tanga Cement kinazalisha zaidi ya tani milioni 1.4 za saruji kwa mwaka, hatua inayochangia ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)