Nchini Colombia, wimbi la vurugu linaendelea kuenea. Tangu Aprili 24, mashambulizi yameongezeka katika eneo la Cauca. Wizara ya Ulinzi imewatambua wapinzani wa FARC chini ya uongozi wa Ivan Mordisco kama waliohusika na shambulio kwenye Barabara Kuu ya Pan-American siku ya Jumamosi, Aprili 25, ambalo lilisababisha vifo vya watu 19 na 48 wakiwa kujeruhiwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Medellín, Najet Benrabaa

Kutokana na dharura hiyo, serikali iliitisha kikao kisichokuwa cha kawaida cha baraza la usalama, na sasa inatoa hadi peso bilioni 5 kwa taarifa yoyote itayopelekea kukamatwa kwa wahalifu.

Katika saa 48, jumla ya mashambulizi 26 yalirekodiwa kote nchini. Waziri wa Ulinzi, Jenerali Pedro Sánchez, alisafiri hadi jimbo la Cauca kusimamia zoezi la kutumwa kwa wanajeshi katika jimbo hilo.

Alihutubia vyombo vya habari: “Mashambulizi haya ni uthibitisho wa udhaifu na woga wa wapinzani wa FARC, ambao wanahisi wamenaswa baada ya mashambulizi yetu ya kijeshi dhidi yao katika jimbo la Cauca na kwenye mpaka na Valle del Cauca. Tutaimarisha uwepo wetu na vikosi viwili vya kivita. Watawasili na vifaa vya ziada vya kiteknolojia kwa ajili ya ufuatiliaji na kuzuia. Tunaimarisha idara zetu za ujasusi ili kuwafuatilia wale waliohusika na mashambulizi hayo, ambapo mhusika mkuu ni yule aliyepewa jina la utani Marlon.”

Tangu kuvunjika kwa mazungumzo ya amani na serikali miezi kadhaa iliyopita, kundi hili limetangaza rasmi vita dhidi ya mamlaka. Mashambulizi hayo yanaendelea kusababisha waathiriwa kote nchini.

Wiki chache tu kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais, mvutano umefikia kiwango kipya. Eneo la Cauca limetangaza siku tatu za maombolezo kama kutoa heshima kwa waathiriwa wa mashambulizi hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *