
Gazeti la Kimarekani la New York Times limemtaja Donald Trump kuwa ndiye rais mbaya zaidi katika historia ya Marekani.
Likielezea madhara makubwa na yasiyo ya kawaida yaliyosababishwa na Donald Trump kwa taasisi za umma na za binafsi, kaida za kidemokrasia, mfumo wa mahakama na vyuo vikuu ndani ya Marekani, pamoja na mahusiano ya nchi hiyo na washirika wake duniani, gazeti la New York Times limeandika katika ripoti yake ya uchambuzi kwamba: “Yeye ndiye rais mbaya zaidi katika historia ya Marekani.”
Ripoti hiyo imesema: Trump, kwa kupunguza bajeti ya Taasisi ya Kitaifa ya Afya, amefuta majaribio ya kimatibabu ambayo yamesababisha vifo vya mapema vya wagonjwa wengi wa saratani.
Katika sehemu nyingine ya uchambuzi wake, New York Times pia limeandika: Trump kwa sasa amejikuta katika hali ambayo njia yoyote atakayochukua—iwe kuzidisha vita dhidi ya Iran au kurudi nyuma—ina gharama kubwa. Mgogoro huu umekuwa njia panda hatari kwake ambayo si rahisi kutoka.
Gazeti hilo la Marekani limeongeza: “Trump alianza vita dhidi ya Iran kwa ahadi za uongo za Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa Israel, lakini mambo hayakwenda kama alivyoahidiwa, na ndoto zote zilibatilishwa na mapambano ya kushangaza ya Iran. Sasa, baada ya karibu miezi miwili, Trump anahangaika kujitoa kwenye kinamasi hicho.”