‎#HABARI: Bodi ya Korosho Tanzania imeanza zoezi la kusambaza viwatilifu vya maji katika Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, huku kipaumbele kikielekezwa kwenye maeneo ambayo korosho huchipua mapema ikiwemo Kata ya Kitama.

Msimamizi wa usambazaji pembejeo kutoka Bodi ya Korosho, Shuma Mpore, ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuwafikia wakulima kwa wakati ili kuimarisha uzalishaji wa zao hilo kulingana na msimu unavyoanza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Ahmadi Katani, ameishukuru Serikali kwa kuwahi kufikisha pembejeo hizo ambazo ni muhimu kwa ustawi wa zao la korosho.

Aidha, Afisa Kilimo wa Tarafa ya Mihambwe, Omary Njwayo, amebainisha kupokelewa kwa idadi ya kutosha ya viwatilifu katika eneo lake, hatua inayowapa wakulima matumaini ya kukabiliana na visumbufu vya mazao na kuongeza tija katika mavuno yao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *