
Ufaransa inawashauri raia wa Ufaransa walioko Mali “kupanga kuondoka kwa muda haraka iwezekanavyo kwenye ndege za kibiashara ambazo bado zinapatikana,” kulingana na maagizo yaliyosasishwa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje yaliyochapishwa Aprili 29. Kundi la Azawad Liberation Front linatoa wito kwa wanamgambo wa Urusi kutoka Africa Corps kuondoka nchini.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Baada ya mashambulizi ya Jumamosi, Aprili 25, 2026, katika maeneo kadhaa nchini Mali, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Mali, Bamako, hali ya usalama bado ni tete,” Wizara ya Mambo ya Nje ilisema siku ya Jumatano. “Kama ukumbusho, inashauriwa kutokwenda Mali, hata kwa sababu yoyote ile,” Quai d’Orsay imekumbusha, ikiongeza: “Katika muktadha huu unaobadilika, raia wa Ufaransa ambao bado wako Mali wanahimizwa sana kubaki nyumbani na kuwasiliana na familia zao na wapendwa wao, wakiwapa taarifa mara kwa mara.”
Kwa jumla, raia 4,200 wa Ufaransa wamesajiliwa na ubalozi, na wale ambao hawajasajiliwa, wanaokadiriwa kuwa takriban 3,000. Theluthi mbili kati yao ni raia wenye uraia pacha wanaoishi katika mji mkuu wa Mali.
Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Mali, Jenerali Assimi Goïta, alijitokeza tena kwenye televisheni ya kitaifa mnamo Aprili 28, akisema kwamba hali, ambayo aliielezea kama “mbaya zaidi,” “imedhibiiwa” na jeshi.
Hali bado ni tete nchini Mali kufuatia mashambulizi yaliyoratibiwa Aprili 25 na 26 na wanajihadi kutoka kundi linalodai kuunga mkono Uislamu na Waislamu (JNIM) na Azawad Liberation Front (FLA) dhidi ya miji kadhaa. Wakati wa mashambulizi haya, Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara aliuawa, na vikosi vya waasi vilichukua udhibiti wa Kidal.
Waasi watangaza kwamba utawala wa kijeshi “utaanguka mapema au baadaye”
Utawala wa kijeshi wa Mali, “utaanguka mapema au baadaye” licha ya mashambulizi ya pamoja ya wapiganaji wa wanajihadi na waasi wanaotaka kujitenga wa Tuareg kutoka Azawad Liberation Front (ALF), msemaji wa kundi hili la waasi alliambia shirika la habari la AFP mnamo Aprili 29, 2026. “Kutokana na mashambulizi ya ALF yenye lengo kudhibiti eneo la Azawad (kaskazini mwa Mali) upande mmoja, na mashambulizi ya wengine (wapiganaji wa kundi la kijihadi la JNIM) huko Bamako na miji mingine, hawataweza kuvumilia,” alisema Mohamed Elmaouloud Ramadane, wakati wa ziara yake Paris. “Tayari tumeikomboa Kidal. Taoudénit ilikuwa tayari chini ya udhibiti wetu. Gao, Timbuktu, na Ménaka pia zitakuwa malengo yetu yanayofuata ya kuzikomboa,” aliongeza. Mohamed Elmaouloud Ramadane pia alisisitiza kwamba “lengo lao ni kwa Urusi kujiondoa kabisa kutoka Azawad na, zaidi ya hayo, kutoka nchi kote Mali.”
Walikuwa wamezingirwa, kwa hivyo waliomba walindiwe usalama ili waweze kuondoka. Walisindikizwa hadi Annefis, na sasa wanawasubiri washirika wao huko Aguelhok na Tessalit. Natumai wataondoka kabisa katika miji yote ya Azawad, na kwa kweli, nchini kote Mali…