Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limechapisha ripoti yake siku ya Alhamisi, Aprili 30, ikielezea vurugu za baada ya uchaguzi nchini Uganda, zilizofuata kuchaguliwa tena kwa rais Yoweri Museveni kwa muhula wa saba mfululizo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo  lisilo la kiserikali linalaani ukandamizaji uliolenga wafuasi wa upinzani, katika muktadha wa vikwazo vikali vyombo vya habari. Ingawa ghasia hazionekani sana kama ilivyo katika nchi zingine katika eneo hilo, vurugu hizo ni za kweli na za kutisha sana, kulingana na shirika hilo.

Ikilinganishwa na mwaka 2021, vurugu nchini Uganda zilikuwa za juu na zililenga zaidi wafuasi wa upinzani—haya ndiyo matokeo makuu ya utafiti, unaoungwa mkono na mashahidi, kuhusu vurugu za baada ya uchaguzi uliochapishwa na shirka la Amnesty International. Kulingana na shirika hilo lisilo la kiserikali, ukandamizaji huo uliwalenga zaidi wafuasi wa upinzani, haswa wale wa chama cha National Unity Platform (NUP).

“Kiwango cha ukatili dhidi ya chama kikuu cha upinzani, NUP, hakijawahi kutokea,” anasema Sikula Oniala, mtafiti wa Amnesty International kwa Tanzania na Uganda, akizungumza na Christina Okello, mwandishi wa habari katika kitengo cha RFI kanda ya Afrika. “Huko Butambala, katikati mwa nchi, angalau watu saba waliuawa nyumbani kwa mbunge, Muwanga Kivumbi, baada ya shambulio la jeshi. Idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi.”

“Ukiukaji huu unabaki kuwa wa kutisha sana.” Kiwango cha vurugu ambacho baadhi hukiona kuwa hakionekani sana kuliko katika nchi jirani kama Tanzania. Hoja iliyokataliwa na Sikula Oniala, ambaye anapendekeza ukandamizaji wa siri zaidi, haswa kutokana na vikwazo vya ufikiaji wa intaneti.

“Uganda inaonekana imejifunza kutokana na kile kilichotokea Tanzania kwa kuzima intaneti mapema.” Mashahidi pia waliripoti milio ya risasi iliyoendelea katika maeneo kadhaa, ambayo iliwazuia wakazi kuondoka majumbani mwao. “Ukiukaji huu unabaki kuwa wa kutisha sana,” mtafiti alibainisha.

Miezi minne baada ya uchaguzi, wanachama kadhaa wa upinzani bado nazuiliwa, na baadhi ya wafuasi wa NUP wanasema wanaishi kwa hofu ya kulipizwa kisasi. Amnesty International sasa inatoa wito wa uchunguzi na mashtaka kwa wale waliohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *