
Mahakama ya kijeshi nchini DRC inatafuta kuthibitisha tena nidhamu ndani ya vikosi vya jeshi vya nchi hiyo. Zaidi ya wanajeshi 80 wa FARDC wanashtakiwa, huko Kisangani, kwa “uasi,” “kukataa kupigana,” na “kuuza vifaa vya kijeshi” mapema mwaka huu, katika jimbo la Tshopo. Matukio haya yalitokea Pinga, katika eneo la Walikale la Kivu Kaskazini, katikati ya mvutano unaohusiana na malipo ya bonasi wakati wa vita vinavyoendelea dhidi ya waasi wa AFC/M23, ambao wanaungwa mkono na jeshi la Rwanda.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Kesi hiyo ilifunguliwa siku ya Jumatano, Aprili 29, mbele ya mahakama ya kijeshi huko Kisangani. Wanajeshi themanini na wanne kutoka kitengo kilichowekwa katika eneo la Walikale wanashtakiwa kwa “uasi,” “kukataa kupigana,” na “kuuza vifa vya jeshi.”
Kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa DRC, matukio hayo yanaanzia mwezi Februari katika mji wa Pinga ambapo wanajeshi hawa walikataa kupigana, wakitaja, miongoni mwa mambo mengine, kutolipwa kwa bonasi zao. Hii ilifuatiwa na urushaji wa risasi mjini humo. Malalamiko ya pamoja ambayo ni marufuku kabisa ndani ya safu za jeshi.
Kesi ya kilimu na kuzuia wanajeshi kuendelea kuasi
Kamanda wa kanda ya Tatu ya Ulinzi aliwasilisha kesi mahakamani, akitumai kesi ambayo itakuwa ya kielimu na ya kuzuia wanajeshi wote kuasi. Kikao cha kwanza kilihusu tu kuwatambua wafungwa kabla ya uchunguzi rasmi kuanza siku ya Jumatatu.
Wakili wa upande wa utetezi alitaja ukosefu wa ushahidi na akasema tangu mwanzo kwamba “kesi hii inavuruga utulivu kwa jeshi.” Wanajeshi hawa, waliozuiliwa kwa miezi miwili katika gereza la kijeshi la Kisangani, wanakabiliwa na kifungo cha maisha jela.