
Mamilioni ya Waingereza wanapiga kura leo Alhamisi katika uchaguzi unaotarajiwa kuongeza shinikizo kwa Waziri Mkuu wa Labour ambaye tayari amedhoofika, Keir Starmer, na kuonyesha kuongezeka kwa siasa kali za mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wapiga kura nchini Scotland, Uingereza, na Wales wanaenda kwenye uchaguzi kwa kile kitakuwa mtihani mkubwa zaidi wa uchaguzi wa Starmer tangu ushindi wake mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwezi Julai 2024, ambao ulimaliza miaka 14 ya utawala wa Conservative.
Kura za maoni zinatabiri matokeo mabaya kwa Chama cha Labour, ambayo yanaweza kuongeza wito wa kujiuzulu kwa Starmer, 63, au kumsukuma hatimaye kukabiliana na changamoto ya uongozi iliyojadiliwa kwa muda mrefu.
Chama cha Nigel Farage kinachopinga kupinga uhamiaji cha Reform UK na chama cha Greens, kinachoongozwa na Zack Polanski anayejitangaza kuwa mwanaharakati wa mazingira, vinatarajiwa kuwa wanufaika wakuu uchaguzi huu.
“Hiki ni kiashiria muhimu cha jinsi nchi inavyohisi kuhusu wanasiasa wa sasa,” amesema Melanie Garson, Profesa mshiriki wa siasa katika Chuo Kikuu cha London , University College London.
“Kwa mara ya kwanza, vyama vikuu vya siasa vinakabiliwa na shinikizo kubwa katika kila baraza la serikali za mitaa.”
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa saa 1 asubuhi (8 asubuhi saa za Ufaransa) na kufungwa saa 4 usiku. Baadhi ya matokeo yanatarajiwa usiku , lakini mengi yatajulikana siku ya Ijumaa alasiri.
Takriban viti 5,000 vya baraza la setikali za mitaa, kati ya 16,000, vinapigiwa kura kote Uingereza, huku wapiga kura wa Wales na Scotland wakichagua mabunge mapya ya ugatuzi
Starmer aliingia madarakani miaka miwili iliyopita baada ya miaka 14 ya serikali ya kihafidhina iliyokumbwa na machafuko makubwa, kufuatia hatua za kubana matumizi, Brexit, na kushuka kwa uchumi chini ya Waziri Mkuu wa zamani Liz Truss.
Lakini wakosoaji wake wanasema amefanya mfululizo wa makosa ya kisiasa na amejikuta katika kashfa inayomhusisha mjumbe wa zamani wa Marekani Peter Mandelson, mshirika wa Jeffrey Epstein, aliyefariki, ambaye alikuwa mfadhili na mfanyabiashara tajiri wa Marekani ambaye alijulikana kama mhalifu wa kingono aliyepanga mtandao mkubwa wa usafirishaji wa binadamu na unyanyasaji wa kingono wa wasichana wadogo.
Starmer pia ameshindwa kutimiza ahadi yake kuu ya kufufua ukuaji wa uchumi, huku Waingereza wasio na subira wakiendelea kuteseka kutokana na mgogoro wa gharama za maisha, hasa kutokana na kupanda kwa bei za nishati.