Narges Mohammadi, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kutoka Iran aambaye anafungwa, amehamishiwa hospitalini huko Tehran na mamlaka imeamua kusitisha kifungo chake kwa dhamana ya juu, taasisi inayoendeshwa na familia yake imetangaza Jumapili, Mei 10.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Akiwa na umri wa miaka 54, Narges Mohammadi alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2023 akiwa gerezani kwa kufanya kampeni ya haki za wanawake na kufutwa kwa adhabu ya kifo. Alipata mshtuko wa moyo wiki mbili zilizopita.

Familia yake ilikuwa imeomba ahamishwe kutoka Zanjan, kaskazini magharibi mwa Tehran, ambapo alikuwa akitumikia kifungo chake na ambapo hapo awali alikuwa amelazwa hospitalini, ili aweze kupata huduma bora za kimatibabu.

Sasa yuko katika Hospitali ya Pars huko Tehran, ambapo anatunzwa na timu yake ya matibabu, Wakfu wa Narges Mohammadi umesema katika taarifa.

“Kusitishwa kwa kifungo hakutoshi” 

Narges Mohammadi alihukumiwa kifungo cha miaka saba na nusu jela mwezi Februari, wiki chache tu kabla ya Marekani na Israel kuanza vita vyao dhidi ya Iran. Kamati ya Nobel kisha iliitaka Tehran kumwachilia mara moja.

Wakfu huo haukutoa maelezo yoyote kuhusu masharti ya kuachiliwa kwake kwa dhamana au kusitishwa kwa kifungo chake. “Hata hivyo, kusitishwa kwa kifungo hakutoshi,” imesema Kamati ya Nobel. “Narges Mohammadi anahitaji huduma maalum inayoendelea. Tuwe na mani kwamba hatarudi gerezani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *