Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanamke aliyefahamika kwa jina la Aisha Miraji mkazi wa Nzasa Temeke.

Mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa kwenye maji eneo la daraja la Salender, Ilala le Jumatatu, Mei 11, 2026 saa 4:30 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mwili huo haukuonekana kuwa na jeraha lolote la wazi na kwamna uchunguzi wa awali umebaini kuwa Aisha alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili Mei 10, 2026 akiwa pamoja na wazazi wake kabla ya kupotea ghafla.

Wazazi wa marehemu wameeleza kuwa mtoto wao alikuwa akisumbuliwa na changamoto za kiafya kwa nyakati tofauti ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita na kwamna linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mazingira halisi yaliyopelekea kifo hicho.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *