Iraq yachora mstari mwekundu; yasema: Ardhi ya nchi hiyo haitatumika kufanya mashambulizi dhidi ya Iran au nchi jiraniIraq yachora mstari mwekundu; yasema: Ardhi ya nchi hiyo haitatumika kufanya mashambulizi dhidi ya Iran au nchi jirani

Iraq imetangaza wazi kuwa kamwe haitaruhusu ardhi yake itumike kwa ajili ya kufanya mashambulizi dhidi ya nchi jirani, hasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sabah al-Numan, Msemaji wa Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iraq, jana alisisitiza kuwa Baghdad imepitisha sera ya wazi ya kujiweka mbali na mihimili ya migogoro ili kulinda amani na utulivu nchini humo.

“Hatutaruhusu Iraq kutumika kama sehemu ya kutekelezea mashambulizi dhidi ya nchi nyingine,”amesema al-Numman. Aidha amesisitiza kuwa Iraq haitaunga mkono mashambulizi yoyote ya kigeni kwenye ardhi yake au kuingiliwa katika masuala yake ya ndani.

 Al- Numan amesema kuwa, chaguo sahihi la kimkakati la Iraq ni kuepuka kujifungamanisha na kambi za mizozo ya kikanda na kimataifa kama hatua muhimu ya kukudumisha utulivu wa ndani.

Ameema doktrini ya usalama na kisiasa inayosimamia mpango wa serikali imejikita katika diplomasia ya kuzuia na kusimamia kwa usawa mahusiano ya kimataifa.

Msimamo huu wa msingi ulipata nguvu mwezi Machi mwaka huu wakati Waziri Mkuu Mohammed Shia al-Sudani alipomhakikishia Rais wa Iran Masoud Pezeshkian kwamba hakuna upande wowote utakaoruhusiwa kutumia ardhi ya Iraq kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *