Wizara ya Mambo ya nje ya Iran, inasema viongozi wake, wanapitia majibu mapya ya Marekani kuhusu upatikanaji wa mkataba wa amani, baada ya awamu kadhaa ya mazungumzo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hilo limesemwa na Esmaeil Baghaei, msemaji wa Wizara hiyo, wakati huu mazungumzo yakiendelea.
Naye kiongozi wa kiroho wa Iran Mojtaba Khamenei, ameripotiwa kuagiza kuwa urutubishaji wa madini ya Uranium ili kutengeza silaha uendelee nchini humo, badala ya kuhamishiwa katika nchi nyingine.
Iran kwa sasa ina Kilogramu 400 ya uranium iliyorutubishwa, ambayo Israeli inasema inaweza kutengeneza mabomu 11 ya nyuklia.
Haya yanajiri wakati huu Pakistan ikiongoza mazungumzo ili kupata mkataba kati ya Iran na Marekani, utakaomaliza vita katika eneo la Mashariki ya Kati.
Katika hatua nyingine, tume mpya iliyoteuliwa na mamlaka nchini Iran kusimamia shughuli kwenye eneo la Bahari la Hormuz, inasema kwa sasa inadhibiti hadi katika bahari ya Emirati.
Tangu kuanza kwa vita mwezi Februari, safari za meli katika eneo la Hormuz zimesitishwa, huku eneo hilo likiwa chini ya usimamizi wa Iran.
