Nigeria: Vyama vya siasa kuanza kuwateuwa wagombea urais kuelekea uchaguzi mkuuNigeria: Vyama vya siasa kuanza kuwateuwa wagombea urais kuelekea uchaguzi mkuu

Nchini Nigeria, vyama vya siasa kuanzia siku ya Jumamosi, vitaanza zoezi la kuwateuwa wagombea urais kuelekea uchaguzi mkuu, uliopangwa kufanyika mwezi Junauari mwaka ujao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Chama tawala All Progressives Congress (APC) kinatarajiwa kumteua tena rais Bola Tinubu, mwenye umri wa miaka 73, kuwania uongozi wa taifa hilo lenye watu wengi barani Afrika kwa muhula wa pili.

Muhula wa kwanza wa Tinubu, umekumbwa na changamoto nyingi za kiuchumi, kufuatia mageuzi ambayo wachambuzi wanasema, yamesaidia kuimarisha uchumi wa nchi hiyo licha ya kusabisha kupanda kwa gharama ya maisha.

Suala la utovu wa usalama, hasa maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo, ni jambo lingine ambalo limeendelea kutatiza uongozi wake, licha ya ahadi ya kumaliza changamoto hiyo.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Nigeria
Mwanasiasa wa upinzani nchini Nigeria AP – Mosa’ab Elshamy

Uteuzi huu unakuja wakati vyama vya siasa vya upinzani, vikionekana kugawanyika suala ambalo wachambuzi wa siasa wanasema, litamsaidia rais Tinubu kuchaguliwa tena kwa urahisi.

Chama kikuu cha upinzani cha PDP ambacho kiliwahi kuongoza nchi hiyo kwa miaka 16, kinaonekana kugawanyika kwa makundi mawili, huku kile cha Leba kikionekana kuvunjika kabisa.

Muungano wa chama cha African Democratic Congress (ADC), kinachowaleta pamoja wanasiasa Peter Obi, Atiku Abubakar na  Rabiu Kwankwaso , wanaonekana kutokuwa tena pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *