Timu za taifa zapigwa tafu miaka miwiliTimu za taifa zapigwa tafu miaka miwili

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya usambazaji vinywaji baridi, Watercom kwa ajili ya timu zote za Taifa.

Hatua hiyo imemuibua Rais wa TFF, Wallace Karia ambaye amesema itazisaidia timu za taifa zikiwa na mashindano mbalimbali.

“Ni jambo zuri kupata wadhamini tofauti wa kuwekeza kwa timu zetu za taifa zinapokuwa katika majukumu, tunashukuru kwa udhamini huu,” amesema Karia. 

Kwa upande wa mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mohammed Salum, ameweka wazi mkataba huo una thamani ya Sh70 milioni, lakini gharama inaweza kuongezeka kulingana na mashindano.

MKAT 01

“Mkataba wetu unajikita katika matumizi, hivyo kama mashindano yatakuwa mengi basi gharama zitaongezeka, lengo ni kusapoti timu zetu za taifa ili kuendelea kufanya vizuri,” amesema.

Mkataba huo umekuja wakati ambao timu ya taifa ya Tanzania maarufu Taifa Stars inajiandaa kucheza mechi za kirafiki za kimataifa zilizopo katika kalenda ya FIFA dhidi ya Rwanda na Uganda.

MKAT 02

Pia, Taifa Stars imepangwa Kundi L katika mechi za kufuzu AFCON 2027 ikiwa na timu za Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau. Mechi hizo zitaanza Septemba 21, 2026 hadi Machi 30, 2027, kabla ya mashindano yenyewe kuanza Juni 19 hadi Julai 17, 2027 ambapo Tanzania ni nchi mwenyeji kwa kushirikiana na Uganda na Kenya.

Mbali na hilo, Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, ipo Morocco ikishiriki Fainali za AFCON U-17 ikitinga nusu fainali ikitarajiwa kucheza dhidi ya Misri, ikiwa tayari imekata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia U-17, fainali zitakazofanyika Qatar kuanzia Novemba 19, hadi Desemba 13, 2026.

Kama ilivyo kwa Serengeti Boys, pia timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite Queens, nayo imefuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia Wanawake U-20 zitakazofanyika Poland kuanzia Septemba 5 hadi 27, 2026 ikipangwa kundi B na Brazil, England na Canada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *