‎#HABARI: Ujenzi wa Kituo cha Mbegu za Miti ya Miombo kinachogharimu zaidi ya shilingi milioni 500 katika Wilaya ya Kaliua mkoan…‎#HABARI: Ujenzi wa Kituo cha Mbegu za Miti ya Miombo kinachogharimu zaidi ya shilingi milioni 500 katika Wilaya ya Kaliua mkoan…

‎#HABARI: Ujenzi wa Kituo cha Mbegu za Miti ya Miombo kinachogharimu zaidi ya shilingi milioni 500 katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora umekamilika, hatua itakayochochea uzalishaji wa miti imara inayosaidia kupunguza hewa ya ukaa.

Mradi huo unaotekelezwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ufadhili wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), unalenga kuongeza mnyororo wa thamani, kutengeneza fursa za ajira, na kuinua uchumi. Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Gerald Mongella, na Mhifadhi Mwandamizi wa TFS, Sadock Gobanya, wamesema kituo hicho kinaleta matarajio makubwa kwa maendeleo ya wananchi na taifa.

Ujenzi wa kituo cha uchakataji wa mazao ya nyuki nao umeshika kasi wilayani humo ambapo utekelezi wake kwa sasa umefikia asilimia 85 kama ilivyoelezwa na Dkt. Mongella.

Hatua hiyo ya maendeleo imethibitishwa pia na Mkandarasi Mjenzi, Mhandisi Emmanuel Wami, pamoja na Mhifadhi Misitu wa TFS Kaliua, Daudi Swila. Viongozi na wataalamu hawa wamesisitiza kuwa kukamilika kwa miradi hii ya kimkakati mkoani Tabora kutaleta mageuzi makubwa katika uhifadhi wa mazingira na kukuza vipato vya wananchi kupitia sekta ya misitu na nyuki.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *