Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt.BATILDA BURIAN ameunda kamati maalum ya kufuatilia mchakato wa ubomoaji nyumba za wananchi katika kijiji cha Msakangoto kilichopo wilayani Muheza Mkoani humo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt.BATILDA BURIAN amesema ubomoaji huo umeacha Kaya zaidi ya 60 zikiwa hazina makazi na nyumba nyingine zilivunjwa zikiwa na wazee ndani yake bila kujali utu wa wananchi hao.

Aidha ameisisitiza kamati hiyo kufuatilia kujua sababu za kutoshirikishwa kwa Jeshi la polisi pamoja na uongozi wa Mkoa.

Kamati hiyo imepewa muda wa siku tano kuanzia jumatatu ya juni mosi mpaka ijumaa kukamilisha ufuatuliaji huo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *