Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Antananarivo, nchini Madagascar, imeomba idhini ya kuwashtaki majaji wanne wa Mahakama Kuu ya Katiba kwa “njama ya kuhatarisha usalama wa taifa.” Utaratibu huu unakuja siku mbili baada ya mahakama hiyo kutoa uamuzi kuhusu hoja ya kumtimua Kanali Michaël Randrianirina, rais wa chama cha Refoundation.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Madagascar, Aurélie Kouman

Mwendesha mashtaka wa Antananarivo amewasilisha ombi kwa Waziri wa Sheria akitaka kuwashtaki majaji wanne kati ya tisa wa Mahakama Kuu ya Katiba. Shtaka: “njama ya kuhatarisha usalama wa taifa.”

Haikubaliki

Siku mbili mapema, mahakama hiyo iliamua kuwa haikubaliki hoja ya kumtimua Kanali Michael Randrianirina, iliyotolewa na mbunge Antoine Rajerison, ambaye alimtuhumu kwa ukiukaji mkubwa na wa mara kwa mara wa Katiba.

Jana kwenye mitandao ya kijamii, vuguvugu la vijana la “GEN Z”, ambalo kwa kawaida hukosoa sana Mahakama Kuu, lilielezea kushangazwa kwake na mfululizo huu wa matukio. “Je, shinikizo liliwekwa kwa baadahi ya majaji au washauri wakuu?”, vuguvugu hilo linauliza.

Mashitaka

Hali hii inatikea katika mazingira ya wasiwasi yanayozunguka Mahakama Kuu ya Katiba. Siku chache mapema, Bunge la taifa lilijaribu kuteua wabunge wengi kuchukuwa nafasi ya majaji wawili kati ya hawa, ingawa hakuna nafasi yoyote iliyotangazwa katika viti vyao.

Tangu Kanali Randrianirina alipoingia madarakani, kesi za vitisho kwa usalama wa taifa zimeongezeka, zikiwalenga viongozi wa zamani, wapinzani, na wanaharakati wa vuguvugu la vijana la GEN Z. Mahakama Kuu ilipowasiliana na RFI, haikujibu. Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wala Wizara ya Sheria ya Madagaska hawajazungumza chochote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *