
Marekani imetangaza siku ya Jumapili, Mei 31, kwamba imefanya mashambulizi mwishoni mwa wiki kusini mwa Iran, ikilenga mifumo ya rada na udhibiti wa ndege zisizo na rubani, licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya nchi hizo mbili. Siku ya Jumatatu, Juni 1, Kikosi cha walinzi wa mapinduzi kimesema kimelenga kambi inayotumiwa na jeshi la Marekani kwa mashambulizi dhidi ya eneo lao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Marekani imetangaza kutekeleza mashambulizi mapya kusini mwa Iran mwihoni mwa wiki hii iliyopita. Wimbi hili la mashambulizi ya anga ya Marekani, la tatu katika kipindi cha zaidi ya wiki moja, lililenga jiji la Goruk na Kisiwa cha Qeshm karibu na Mlango wa Hormuz, Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imebainisha kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Operesheni hizi zilifanywa “siku ya Jumamosi na Jumapili kujibu vitendo vya uchokozi vya Iran, ambapo ndege isiyo na rubani ya Marekani ya MQ-1 iliyokuwa ikiendesha shughuli zake juu ya maji ya kimataifa, iliangushwa,” chanzo hicho kiliongeza, wakati ambapo mazungumzo kati ya Washington na Tehran ili kukomesha vita vilivyoanza Februari 28, yamekwama.
Kikosi cha walinzi wa mapinduzi kimesemaleo Jumatatu Juni 1, 2026 kuwa kililenga kambi inayotumika kwa mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya eneo lake.
Mahali pa kambi hii hakutajwa katika taarifa ya Kikosi cha walinzi wa mapinduzi iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.