Katibu wa NEC Itikadi uenezi na mafunzo CCM Taifa Kenani Kihongosi ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa shule ya Sekondari Beselo iliyopo Babati Vijijini ambayo imetajwa kuwa itasaidia wanafunzi kupata elimu bora katika mazingira safi na salama

Kihongosi ametoa ujumbe huo wakati wa ziara hiyo Mkoani Manyara yenye lengo la kufuatilia uhai wa Chama na utekelezaji wa mradi ya maendeleo ambapo ameeleza kuridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa mradi huo na kupongeza uongozi wa shule kwa usimamizi mzuri.

Aidha ametoa pongeza kwa viongozi wa mkoa wa Manyara kwa kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya maendeleo .

Amesisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kitaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuleta mageuzi makunwa ya kiuchumi na kijamii

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *