Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini kwa Watoto, Dkt. Livin Mumburi, amesema watu wengi hukosa watu wa karibu wa kuwapa moyo katika safari zao za mafanikio, jambo ambalo huwakatisha tamaa katika kufikia ndoto zao.
Amesema kujifunza kwa watu waliofanikiwa husaidia kuimarisha imani kuwa mafanikio yanawezekana, mradi mtu awe na malengo na uthubutu.
Ameeleza kuwa safari yake ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya ini na mfumo wa chakula kwa watoto imetimia kutokana na msaada na motisha kutoka kwa watu wa karibu waliomwonesha kuwa inawezekana kufanikisha malengo yake.
Amesema vijana wanapaswa kutumia mifano ya watu waliofanikiwa kama chachu ya kujenga imani na kupambana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
✍ Ibrahim Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
@goodluckpaul_mc
@balqis_njuki
#AzamTVupdates
(Feed generated with FetchRSS)