Chanzo cha picha, Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2
Bruno Guimaraes ameomba kuondoka Newcastle, huku Arsenal ikiongeza kasi ya nia yake ya kumsajili kiungo huyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Lyon mwaka 2022, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England katika dirisha hili la usajili la majira ya joto.
Arsenal ilikuwa ikitathmini uwezekano wa kumsajili Guimaraes au mchezaji mwenzake wa zamani, Sandro Tonali — ambaye sasa amejiunga na Tottenham kwa ada ya awali ya pauni milioni 92.5 — katika juhudi zao za kuimarisha safu yao ya kiungo.
Manchester United wanalenga kupanga uhamisho wa mshambuliaji wao wa England, Marcus Rashford (28), kabla ya kambi yao ya mazoezi ya kabla ya msimu kuanza jijini Dublin mwezi Agosti. (Sun)
Hata hivyo, kuna mipango pia ya kumrejesha Rashford katika kikosi cha Manchester United chini ya kocha Michael Carrick. (Guardian)
Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal na Tottenham ni miongoni mwa klabu tano za Ligi Kuu ya England zinazomnyatia winga wa RB Leipzig na Norway, Antonio Nusa (21). (Teamtalk)
Barcelona wamemjumuisha mshambuliaji Mfaransa wa Bournemouth, Eli Junior Kroupi (20), kwenye orodha yao fupi, lakini wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain, Arsenal na Tottenham. (Fichajes – In Spanish)
Juventus wanataka Aston Villa kupunguza bei wanayotaka ya euro milioni 10 (pauni milioni 8.5) kwa ajili ya kipa wa Argentina, Emiliano Martinez (33), baada ya tayari kufikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo. (La Gazzetta dello Sport – In Itali)
Barcelona wanashindana na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England, zikiwemo Chelsea, Manchester City na Manchester United, kumsajili beki anayesifiwa sana wa Colorado Rapids na Australia, Lucas Herrington (18). (Teamtalk)
Manchester City, Arsenal na Liverpool wote wanamwania kiungo wa Lille mwenye umri wa miaka 18, Ayyoub Bouaddi, ambaye anang’ara katika Kombe la Dunia akiichezea Morocco. (Football Insider)
Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea watazingatia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Serbia, Dusan Vlahovic (26), iwapo wataamua kuboresha safu yao ya ushambuliaji msimu huu wa joto. (CaughtOffside)
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho, anawafikiria Riccardo Calafiori (24) wa Arsenal na Italia, Piero Hincapie (24) wa Chile (ambaye ni mwenzake Calafiori), na Ruben Dias (29) wa Manchester City na Ureno, huku akitaka kuongeza nguvu na umbile imara katika safu ya ulinzi ya timu yake. (Fichajes – In Spanish}
Kiungo wa zamani wa Liverpool na Brazil, Fabinho (32), anasema ana nia ya kuungana tena na Mourinho huko Real Madrid baada ya kuondoka Al-Ittihad. (Talksport),
Sporting wanatarajiwa kumsajili Jesse Derry wa Chelsea, mwenye umri wa miaka 19, kwa mkopo wa msimu mzima, huku winga huyo akitarajiwa kuwasili Lisbon kwa ajili ya vipimo vya afya. (Sky Sports)