Wafanyabiashara katika soko kuu la Tunduru mkoani Ruvuma wamelalamikia hali ya miundombinu katika soko hilo, wakisema mazingira yaliyopo yanaweza kuhatarisha ubora wa bidhaa zao, hususan vyakula, pamoja na usalama wa walaji.
Wafanyabiashara hao wameeleza kutoridhishwa na hatua ya Halmashauri kuendelea kuongeza kodi za vibanda vya soko bila kuwashirikisha, huku wakidai kuwa ahadi ya ujenzi wa soko jipya bado haijatekelezwa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)