HABARI: Makabiliano yameshudiwa katika kanisa alikokuwa anahudhuria aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua ibaada ya Jumapili katika Kanisa la ACK Wairima eneo la Othaya kaunti ya Nyeri. Polisi waliokuwa wamefunika nyuso zao wametupa mabomu ya kutoa machozi katika kanisa alikokuwa Gachagua.
Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya mabomu ya kutoa machozi kutupwa kanisani. Gachagua amefanikiwa kutoroka kupitia ua wa Kanisa hilo.
(Feed generated with FetchRSS)