#HABARI: Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. John Mongella, amewataka viongozi wa chama hicho kote nchini, kuhakikisha mashina na matawi yanapewa kipaumbele na kusisitiza kuwa mashina na matawi ndiyo msingi wa maendeleo ya wananchi na uhai wa chama.

Bw. Mongella ameyasema hayo wakati wa ziara yake kata ya Kagongwa mkoani Shinyanga, ambapo alikagua uhai wa chama na kuongoza shughuli za upandaji miti katika ofisi ya CCM kata hiyo, shughuli hiyo ni sehemu ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi.

Ziara hiyo ya siku nne mkoani Shinyanga inalenga kukagua uhai wa chama pamoja na kutatua changamoto na kero zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *